Wedding, Event, Conference Photography and Videography

We offer all types of Photography ranging from, Wedding, Event, Conference, Model Photoshoot, special occasion, Birthday Party, Funeral, Movie, Filming and others.

Graphics Designing

We are expertised from Deigning, Developing and Printing Images generated from Computer Software by Using Special Graphics editing Application.

Web Experts

Our Team is Dedicated to provide Web Designing, Hosting, Development and Maintenance using many of the known Internet Applications, Web languages and Connectivity Software.

Brand Advertizing and Marketing

We Brand your company, Advertise your Products and give you great results of where, how, when to increase your sales and make more profits.

Social Media Management

Our customer's Social network is our playground.This is where we meet and bring people together to Brain Storm.

Monday, February 25, 2013

Steve Nyerere


Steve Nyerere asababisha ajali ya Gari, atupwa Lupango.



Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Steve Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo (jana) imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi (jana).

Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hiyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.





Wasanii hao pamoja na Steve, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.

Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- 
Wakati Steve akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti scenes zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.


Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.


Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.


Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.


Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Steve na Askari huyo, aliyediriki kumuita Steve mjinga, ambapo Steve alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.